BIASHARA YAKO INAKUTEGEMEA WEWE.
Zama za kuanzisha biashara na kukaa kusubiria wateja waje, zimepitwa na wakati. Sikia, Ushindani katika biashara umekuwa mkubwa sana na una hatarisha biashara nyingi zinazomilikiwa na watu ambao siyo wabunifu hasa katika kutafuta masoko. Mawazo ya biashara yamekuwa ni ya kujirudiarudia mwisho wa siku unakuta biashara moja inafanywa na watu kumi eneo moja. Unafanya biashara umezungukwa na washindani wengi kiasi hicho hapo ulipo, ulishawahi jiuliza ni kitu gani ufanye ili kujitofautisha na kuongeza mauzo? Au unaona ni sawa tu yaani ukipata mteja mmoja au wawili kwa siku kwako sawa tu! Na unamuomba Mungu angalau upate mteja mmoja kwa siku?!!
Hivi wewe na biashara yako ulishawahi
kaa kujiuliza uongeze au kupunguza nini ili KUJITOFAUTISHA?? Yes, nazungumzia
KUJITOFAUTISHA, kwa lugha rafiki ni UBUNIFU, maana hii ndiyo siri kubwa katika
kufanikisha chochote katika biashara yako na hata katika maisha yako kiujumla. Ngoja
nikuambie ndugu yangu, hakuna biashara inayokua kama mmiliki siyo mbunifu na
hata timu yake pia kama hawana ubunifu katika utendaji. HAKUNA! Kampuni zote kubwa unazozijua wewe,
kinachowafanya waendelee kusikikika ni UBUNIFU wanao ufanya kila kukicha.
Nisikuchoshe sana ila naomba nikupe
hili kuhusu DUKA LA MTANDAONI. Unayo smartphone au Computer? Ukiacha kazi ya kupiga
simu na kupokea , kuhifadhi documents zako (Computer), ulishawahi jiuliza ni
namna gani unavyoweza kutumia simu au computer yako kuendesha DUKA LAKO
MTANDAONI na kukuongezea wateja kutoka maeneo mbalimbali ukiacha wale
unaowapata kila siku hapo ulipo?
Ngoja, nikurahisishie bila kuumiza
sana kichwa, Boss unaijua Whattsap? Instagram Je? Blog na Websites nazo
unazitambua au unazionaga tu na kuzipotezea??!! Ok tuendelee na vipi kuhusu
Facebook pages? Na hapohapo kwenye facebook, hivi ulishawahi kukutana na
Matangazo ya facebook yaani Facebook Sponsored Ads? Au hayo yote huwa unayapita
tu na uhitaji kuumiza kichwa kujifunza au kujua maana wewe hushakuwa boss na
fremu ipo tayari na hauhitaji chochote cha ziada.
Ebu chukua sekunde kadhaa kutafakari
ni watu wangapi ambao wapo mitandaoni kila siku na wana uhitaji wa huduma
unayoitoa ila hawakuoni mtandaoni, na hawajui hata kuwa upo na unatoa huduma
hiyo, kisha jiulize, nikipanua wigo wa biashara yangu mtandaoni nitapungukiwa
nini?
- Blog bora iliyopangiliwa kwaajili ya huduma au biashara yako.
- Account za mitandao ya kijamii (face
book pages, Instagram, Whattsap Business
na nyine pia kutegemeana na aina ya biashara yako) kufanya settings zote muhimu
na maalum kwaajili ya biashara yako tu.
- Kufanya matangazo facebook (Facebook
Sponsored Ads)
- Kuanzisha youtube channel kwaajili ya huduma yako au biashara yako.
Kwa mfano, wewe unafanya biashara gani?
Au unatoa huduma gani? Je, unadhani wateja unaowaona leo au kwa kipindi hiki
ndiyo hao tu wanaoihitaji bidhaa au huduma yako?
Kuweka biashara yako mtandaoni
unakusaidia na kukupa uwanja wa kuwa na watu wengi sana, ambao miongoni mwao ni
wateja wako wa uhakika vilevile unaweza kutengeneza/kuandaa mkondo endelevu wa
wateja wengi sana wa siku za baadae kwenye biashara au huduma yako.
Usikae kusubiri mteja akutafute, amua
kuwafuata na kuwa nao karibu itakusaidia sana.
Yote niliyokuandikia naelewa kuna
mengine hujui wapi pa kuanzia na mengine hata hujawahi kusikia na kuamini kuwa
yanawezekana. Usihofu tupo kwaajili yako, tunatoa mafunzo bure kabisa na kama
utahitaji kutengenezewa Blog, Page bora za biashara facebook, Instagram,
youtube, kufanyiwa setting na jinsi ya kutumia whattsap business, na huduma
zingine za biashara mtandaoni tunaweza wasiliana kupitia namba 0752026992.
Tunakuhudumia popote ulipo Tanzania. Lengo ni kukutoa hapo ulipo ili ufike sehemu kubwa zaidi. Mabadiliko hayaji kwa kufanya kitu kimoja miaka nenda rudi bila kuongeza au punguza baadhi ya vitu. Amia mtandaoni sasa uone ulimwengu mwingine na ukue zaidi katika biashara yako.
0 Comments